Kwa hiyo Saulo akamwambia mutu aliyemubebea silaha: “Chomoa upanga wako unichome nikufe, kusudi watu hawa wasiotahiriwa wasikuje kunichekelea.” Lakini yule aliyemubebea silaha hakutaka kufanya vile; aliogopa sana. Halafu, Saulo alitwaa upanga wake mwenyewe akauangukia.
Nao watu wa Israeli walioishi katika bonde walipoona waaskari wamekimbia waadui, na kwamba Saulo na wana wake wamekufa, wakahama toka miji yao, wakakimbia. Wafilistini wakaenda na kukaa katika miji hiyo.
Wakamvua nguo, wakatwaa kichwa chake pamoja na silaha zake, halafu wakatuma wajumbe katika inchi yote ya Filistia kutangaza habari kwa sanamu zao na watu.
mashujaa wote wakaondoka na kutwaa mwili wa Saulo na miili ya wana wake, wakaileta mpaka Yabesi. Wakazika mifupa yao chini ya muti wa mwalo kule Yabesi, nao wakafunga kula kwa muda wa siku saba.