Kisha, viongozi wa watu wakakaa katika Yerusalema; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi kwa kuchagua jamaa moja itakayokaa katika Yerusalema, muji mutakatifu. Jamaa zingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.
Na katika miji mingine, watu wa Israeli, makuhani, Walawi, walinzi wa milango na wazao wa watumishi wa Solomono, walikaa katika maeneo yao wenyewe, katika miji yao.
Watu wamoja wa kabila la Yuda na wa kabila la Benjamina walikaa katika Yerusalema: Hawa ndio watu wa ukoo wa Yuda waliokaa Yerusalema: Ataya mwana wa Uzia, mujukuu wa Zakaria mwana wa Amaria mwana wa Sefatia mwana wa Mahalaleli wa uzao wa Peresi;
Watu wa ukoo wa Benjamina waliokaa katika Yerusalema ni: Salu, mwana wa Mesulamu mwana wa Yoedi mwana wa Pedaya mwana wa Kolaya mwana wa Maseya mwana wa Itieli na mwana wa Yesaya.
pamoja na wandugu zao waliofanya kazi katika hekalu walikuwa mia nane makumi mbili na wawili. Pamoja na hao, kulikuwa Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia mwana wa Amsi mwana wa Zakaria mwana wa Pasuri mwana wa Malkiya;
vilevile wandugu zake waliokuwa wakubwa wa jamaa za baba zao; wote pamoja walikuwa watu mia mbili makumi ine na wawili. Vilevile kulikuwa Amasayi, mwana wa Azareli mwana wa Azayi mwana wa Mesilemoti mwana wa Imeri,
na Matania mwana wa Mika mwana wa Zabudi, wa uzao wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba maombi ya shukrani. Bakubukia alikuwa musaidizi wake. Pamoja nao kulikuwa Abuda mwana wa Samua mwana wa Galali wa uzao wa Yedutuni.
Walinzi wa milango waliokaa katika Yerusalema walikuwa: Akubu na Talmoni pamoja na wandugu zao waliokuwa wakilinda milango, walikuwa mia moja makumi saba na wawili.
Kiongozi wa Walawi waliokaa Yerusalema alikuwa, Uzi, mwana wa Bani mwana wa Hasabia mwana wa Matania mwana wa Mika wa ukoo wa Asafu, waliokuwa waimbaji, viongozi waangalizi wa shuguli za nyumba ya Mungu.
Watu wengine walikaa katika miji karibu na mashamba yao. Watu wamoja wa kabila la Yuda walikaa Kiriati-Arba, Diboni na Yekabuseli pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakisi na mashamba yanayouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vinavyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo linalokuwa kati ya Beri-Seba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa Kaskazini.