|
| 1 |
|
| Ninachukia maisha yangu! Malalamiko yangu nitayasema bila kizuizi. Nitasema kwa uchungu wa moyo wangu. |
|
| 2 |
|
| Nitamwambia Mungu: Usinitendee sawa na mwenye makosa. Unijulishe sababu ya kugombana nami. |
|
| 3 |
|
| Ni sawa kwako kunionea, kuzarau kazi ya mikono yako na kupendelea mipango ya waovu? |
|
| 4 |
|
| Uko na macho kama ya mwanadamu? Unaona kama vile mwanadamu anavyoona? |
|
| 5 |
|
| Siku zako ni kama za mwanadamu? Miaka yako kama ya mwanadamu? |
|
| 6 |
|
| Kwa nini unachunguza uovu wangu na kuitafuta zambi yangu? |
|
| 7 |
|
| Wewe unajua kwamba mimi sina kosa, na hakuna wa kuniokoa toka katika mikono yako. |
|
| 8 |
|
| Mikono yako ilinitengeneza na kuniumba, lakini sasa unageuka kwa kuniangamiza. |
|
| 9 |
|
| Kumbuka kwamba uliniumba kwa udongo. Utanirudisha tena katika mavumbi? |
|
| 10 |
|
| Si wewe uliyenimimia kama maziwa, na kunigandisha kama siagi? |
|
| 11 |
|
| Uliuumba mwili wangu kwa mifupa na mishipa, ukaifunika mifupa yangu kwa nyama na ngozi. |
|
| 12 |
|
| Ukanipa uzima na kunitendea mema, ukalinda nafsi yangu kwa uangalifu. |
|
| 13 |
|
| Hata hivyo mambo haya uliyaficha ndani ya moyo. Lakini ninajua kwamba ile ilikuwa nia yako. |
|
| 14 |
|
| Ulikuwa unangojea uone kama nitatenda zambi, kusudi ukatae kunisamehe uovu wangu. |
|
| 15 |
|
| Kama mimi ni mwovu, ole wangu! Kama mimi ni mwenye haki, siwezi kujisifu; maana nimejaa haya, nikiangalia mateso yangu. |
|
| 16 |
|
| Nikiinua kichwa tu, unaniwinda kama simba na kuniponda tena kwa maajabu yako. |
|
| 17 |
|
| Kila mara uko na ushuhuda juu yangu, unaongeza hasira yako juu yangu, unaniletea waadui wapya wanishambulie. |
|
| 18 |
|
| Ee Mungu, kwa nini ulinitoa katika tumbo ya mama? Afazali ningekufa mbele ya watu kuniona, |
|
| 19 |
|
| ningepelekwa katika kaburi, na kuwa kama mutu asiyekuwa. |
|
| 20 |
|
| Siku za maisha yangu si chache? Uniachilie nipate kufurahi kidogo, |
|
| 21 |
|
| mbele ya kwenda kule ambako sitarudi, kule kwenye inchi ya huzuni na giza kubwa; |
|
| 22 |
|
| inchi ya huzuni na fujo, ambako mwangaza wake ni kama giza. |
|
|
|
|