BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kisha Zofari wa inchi ya Namati akamujibu Yobu: |
| 2 |
| Wingi huu wa maneno uachwe tu bila kujibiwa? Mutu wa maneno mengi anaonyesha kwamba hana kosa? |
| 3 |
| Kupapayuka kwako kutanyamazisha watu? Kama ukichekelea watu, hakuna atakayekupatisha haya? |
| 4 |
| Wewe unasema: “Masemi yangu ni safi, mimi sina kosa mbele ya Mungu.” |
| 5 |
| Heri Mungu angefungua kinywa chake na kutoa sauti yake kwa kukujibu! |
| 6 |
| Angekuelezea siri za hekima, maana yeye yuko na maarifa mengi. Ujue kwamba Mungu hakuhesabu makosa yako yote. |
| 7 |
| Unaweza kuvumbua siri za Mungu na kujua ukomo wa Mungu Mwenye Uwezo? |
| 8 |
| Ukubwa wake unapita mbingu; wewe unaweza nini? Kimo chake kinapita kuzimu; wewe unaweza kujua nini? |
| 9 |
| Ukubwa ule unapita urefu wa dunia, unapita upana wa bahari. |
| 10 |
| Kama Mungu akipita, akimufunga mutu na kumuhukumu, nani anayeweza kumuzuia? |
| 11 |
| Mungu anajua watu wasiofaa; anaona uovu vilevile bila magumu. |
| 12 |
| Mupumbafu hawezi kuwa na maarifa. Punda wa pori ni punda wa pori tu. |
| 13 |
| Yobu, ukifanya moyo wako mukamilifu, utainua mikono yako kwa kumwomba Mungu! |
| 14 |
| Kama uovu uko katika mukono wako, uutupilie mbali. Usikubali ubaya ukuwe katika nyumba yako. |
| 15 |
| Halafu utainua uso wako bila kosa, utakuwa imara bila kuwa na hofu. |
| 16 |
| Utazisahau taabu zako zote; utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita. |
| 17 |
| Maisha yako yataangaa kuliko jua la muchana kati, giza lake litabadilika kuwa mapambazuko. |
| 18 |
| Utakuwa na uhakika maana kuna tumaini; utalindwa na kupumzika salama. |
| 19 |
| Utalala bila kuogopeshwa na mutu; watu wengi watakuomba musaada. |
| 20 |
| Lakini waovu macho yao yatafifia, njia zote za kutorokea zitawapotea; tumaini lao la mwisho ni kukata roho! |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/job/011.mp3
42
11