|
| 1 |
|
| Kisha Bildadi, wa inchi ya Suhi, akajibu: |
|
| 2 |
|
| Utawinda maneno ya kusema mpaka wakati gani? Fikiri vizuri nasi tutasema. |
|
| 3 |
|
| Kwa nini unatufanya kama ngombe? Mbona unatuona sisi kuwa wapumbafu? |
|
| 4 |
|
| Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au mawe yahamishwe toka pahali pake? |
|
| 5 |
|
| Kweli, mwangaza wa mutu mwovu utazimishwa; ulimi wa moto wake hautaangaa. |
|
| 6 |
|
| Katika nyumba yake mwangaza ni giza, taa inayomwangazia itazimishwa. |
|
| 7 |
|
| Hatua zake ndefu zitafupishwa; mipango yake itamwangusha chini. |
|
| 8 |
|
| Miguu yake mwenyewe itamutia katika mutego; kila mara anatembea juu ya shimo. |
|
| 9 |
|
| Mutego unamukamata kwenye kisigino, kamba inamunasa kabisa. |
|
| 10 |
|
| Amefichiwa kamba ya kumunasa ndani ya udongo, ametegewa mutego katika njia yake. |
|
| 11 |
|
| Hofu kubwa inamutisha kila upande, inamufuata katika kila hatua yake. |
|
| 12 |
|
| Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imemubana; hasara ziko tayari kumwangusha. |
|
| 13 |
|
| Ugonjwa mukali unakula ngozi yake, ugonjwa wa kifo unaharibu viungo vyake. |
|
| 14 |
|
| Anaongolewa katika nyumba aliyotegemea, na kupelekwa kwa mufalme wa vitisho. |
|
| 15 |
|
| Nyumba yake tupu, wengine wataishi ndani; kiberiti kimetawanywa katika makao yake. |
|
| 16 |
|
| Yeye ni kama muti uliokauka mizizi, matawi yake juu yamenyauka. |
|
| 17 |
|
| Katika inchi hakuna atakayemukumbuka; jina lake halitatamkwa tena katika barabara. |
|
| 18 |
|
| Ameondolewa toka katika mwangaza, akatupwa katika giza; amefukuzwa mbali kutoka katika dunia. |
|
| 19 |
|
| Hana watoto wala wajukuu; hakuna aliyebaki katika makao yake. |
|
| 20 |
|
| Watu wa upande wa magaribi wameshangazwa na yaliyomupata; hofu imewapata watu wa upande wa mashariki. |
|
| 21 |
|
| Hayo ndiyo yanayowapata wasiomujali Mungu; pale ndipo pahali pa wasiomujua Mungu. |
|
|
|
|