BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kisha Yobu akajibu: |
| 2 |
| Hata leo malalamiko yangu ni ya uchungu. Ninapata maumivu na kuugua. |
| 3 |
| Heri ningejua pahali nitakapomupata Mungu! Ningeweza kwenda hata karibu naye. |
| 4 |
| Ningeleta maneno yangu mbele yake, na kumutolea utetezi wangu. |
| 5 |
| Ningeweza kujua atakachonijibu, na kuelewa atakachoniambia. |
| 6 |
| Angeshindana nami kwa nguvu zake zote? Hapana! Bila shaka angenisikiliza. |
| 7 |
| Pale, mutu wa usawa anaweza kujitetea. Mungu, mwamuzi wangu angeamua kuwa sina kosa milele. |
| 8 |
| Ninakwenda mbele, lakini simupati; ninarudi nyuma, lakini siwezi kumwona. |
| 9 |
| Ninamutafuta upande wa kushoto lakini simwoni; ninageukia upande wa kuume, lakini siwezi kumwona. |
| 10 |
| Lakini yeye anajua njia ninayofuata; atakapomaliza kunipima nitatoka mule safi kama zahabu. |
| 11 |
| Ninamufuata kabisa; njia yake nimeishikilia wala sikugeuka pembeni. |
| 12 |
| Sijaacha hata kidogo kushika amri yake; maneno yake nimeyatunza ndani ya moyo wangu. |
| 13 |
| Lakini yeye habadiliki, nani anayeweza kumugeuza? Kitu anachotaka, ndicho anachofanya! |
| 14 |
| Anatimiza yote aliyonipangia; na mengi kama hayo yako katika akili yake. |
| 15 |
| Kwa hivyo, ninatetemeka kwa hofu mbele yake; hata nikifikiri tu ninapatwa na woga. |
| 16 |
| Mungu amefanya moyo wangu uregee, Mungu Mwenye Uwezo amenitia hofu. |
| 17 |
| Maana nimepatwa na giza, na giza kubwa limetanda katika uso wangu. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/job/023.mp3
42
23