BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kisha Yobu akajibu: |
| 2 |
| Aa! Jinsi gani ulivyomusaidia asiyekuwa na uwezo! Jinsi gani ulivyomwokoa asiyekuwa na nguvu! |
| 3 |
| Jinsi gani ulivyomushauri asiyekuwa na hekima, na kumushirikisha ujuzi wako! |
| 4 |
| Lakini umesema hayo kwa ajili ya nani? Nani aliyekusukuma kuongea hivyo? |
| 5 |
| Mizimu kule chini inatetemeka, maji ya chini na wakaaji wake yanaogopa. |
| 6 |
| Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu. Shimo la kuangamia halina kifuniko chochote. |
| 7 |
| Mungu anatandaza kaskazini juu ya pahali patupu, na anatundika dunia pahali pasipo kuwa kitu. |
| 8 |
| Anayafunga maji katika mawingu yakuwe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. |
| 9 |
| Anaufunika uso wa mwezi na kutandaza juu yake wingu. |
| 10 |
| Amechora muviringo juu ya uso wa bahari, penye mpaka kati ya mwangaza na giza. |
| 11 |
| Mungu akitoa sauti ya kukaripa, nguzo za mbingu zinatetemeka na kushangaa. |
| 12 |
| Kwa nguvu zake alituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza Rahabu. |
| 13 |
| Kwa pumzi yake alisafisha anga; mukono wake ulitoboa nyoka mukubwa anayeruka. |
| 14 |
| Ikiwa haya ni machache tu ya matendo yake, ni minongono tu tunayosikia juu yake, nani anayeweza kujua ukubwa wa nguvu yake? |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/job/026.mp3
42
26