Habari Njema 2001
|
| 1 |
| Kisha Elihu akaendelea kusema: |
| 2 |
| “Je, Yobu, unaona jambo hili ni sawa na kufikiri kinyume cha Mungu |
| 3 |
| ukiuliza: ‘Nimepata faida gani kama sikutenda dhambi? Nimefaidika kuliko kama ningalitenda dhambi?’ |
| 4 |
| Mimi nitakujibu wewe, na rafiki zako pia. |
| 5 |
| Hebu zitazame mbingu! Tazama mawingu yaliyo juu kuliko wewe! |
| 6 |
| Ukitenda dhambi, je, Mungu ndiye unayemdhuru? Na kama ukizidisha makosa yako, wadhani unamwumiza? |
| 7 |
| Kama wewe ni mwema, je, unampatia faida, au yeye anapokea kitu kutoka kwako? |
| 8 |
| Uovu wako utamdhuru binadamu kama wewe, wema wako utamfaa binadamu mwenzako. |
| 9 |
| “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia, huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu. |
| 10 |
| Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu, Muumba wangu, mwenye kunifanya niwe mchangamfu usiku, |
| 11 |
| anayetuelimisha kuliko wanyama, na kutufanya wenye hekima kuliko ndege!’ |
| 12 |
| Watu hao huomba msaada lakini Mungu hawajibu, kwa sababu ya majivuno ya watu waovu. |
| 13 |
| Kweli Mungu hasikilizi kilio cha bure; Mungu Mwenye Nguvu hajali kilio hicho. |
| 14 |
| Atakujibu vipi wakati wewe unasema kwamba humwoni na kwamba kesi yako iko mbele yake na wewe unamngojea! |
| 15 |
| Sasa, kwa vile Mungu anazuia hasira yake, wala hajali sana makosa ya watu, |
| 16 |
| Yobu unafungua mdomo kusema maneno matupu, unazidisha maneno bila akili.” |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili2001/job/035.mp3
42
35