|
| 1 |
|
| Kisha Elihu akaendelea kusema: |
|
| 2 |
|
| Univumilie kidogo, nami nitakuonyesha kitu; maana ningali bado na cha kusema kwa ajili ya Mungu. |
|
| 3 |
|
| Nitaleta hekima yangu kutoka mbali sana, na kuonyesha kwamba Muumba wangu ni wa haki. |
|
| 4 |
|
| Kweli maneno yangu si ya uongo; mwenye elimu kamili yuko hapa nawe. |
|
| 5 |
|
| Sikia! Mungu ni mwenye nguvu wala hamuzarau mutu yeyote; uwezo wa akili yake ni mukubwa sana! |
|
| 6 |
|
| Hawaachilii waovu waendelee kuishi; lakini anawapatia wanaoteswa haki zao. |
|
| 7 |
|
| Haachi kuwalinda watu wa haki; nao anawaweka kuwa wafalme watawale na kutukuzwa. |
|
| 8 |
|
| Lakini kama watu wakifungwa minyororo, wakinaswa katika kamba za mateso, |
|
| 9 |
|
| Mungu anawaonyesha matendo yao maovu, na kwamba wao ni watu wenye kiburi. |
|
| 10 |
|
| Anafungua masikio wasikie mafundisho, na kuwaamuru warudi na kuacha uovu. |
|
| 11 |
|
| Wakimutii Mungu na kumutumikia, wanafanikiwa katika siku zao zote; miaka yao yote inakuwa ya furaha. |
|
| 12 |
|
| Lakini wasipomutii, wanaangamia kwa upanga, na kufa kwa kukosa akili. |
|
| 13 |
|
| Waovu wanapenda kukasirika; hawamwombi musaada anapowafunga. |
|
| 14 |
|
| Wanakufa wangali bado vijana, maisha yao yanaisha kama ya washerati. |
|
| 15 |
|
| Lakini Mungu anawaokoa wenye kuteswa kwa mateso yao, anatumia shida zao kwa kuwafumbua macho. |
|
| 16 |
|
| Mungu alikutoa katika taabu, akakuweka pahali pakubwa pasipo shida, na juu ya meza yako amekutayarishia vyakula vizuri. |
|
| 17 |
|
| Lakini sasa umehukumiwa kama mwovu, hukumu ya haki imekupata. |
|
| 18 |
|
| Angalia kasirani isikuvute kwa kuzarau, au usiache ukubwa wa mali za kukukomboa ukupotoshe. |
|
| 19 |
|
| Kilio chako kitafaa kukutoa katika taabu, au nguvu zako zote zitakusaidia? |
|
| 20 |
|
| Usitamani usiku ukuje, ambapo watu wanapotoweka. |
|
| 21 |
|
| Angalisho! Usielekee uovu maana umepewa mateso kwa kukuepusha na uovu. |
|
| 22 |
|
| Kumbuka ukubwa wa uwezo wa Mungu; nani anayeweza kufundisha kama yeye? |
|
| 23 |
|
| Nani basi aliyeweza kumupangia njia yake, au anayeweza kumwambia: “Umekosa”? |
|
| 24 |
|
| Usisahau kusifu matendo yake ambayo watu wameyashangilia. |
|
| 25 |
|
| Watu wote wameona mambo Mungu aliyofanya; mwanadamu anayaona kutoka mbali. |
|
| 26 |
|
| Mungu ni mukubwa sana hata hatuwezi kumujua; muda wa maisha yake hauchunguziki. |
|
| 27 |
|
| Yeye anayavuta kwake maji ya bahari, na kutoka ukungu anafanya matone ya mvua. |
|
| 28 |
|
| Anayafanya mawingu yanyeshe mvua, na kuwatiririshia wanadamu kwa wingi. |
|
| 29 |
|
| Nani anayejua jinsi mawingu yanavyotanda, au jinsi radi inavyonguruma kwake katika anga? |
|
| 30 |
|
| Yeye anatandaza umeme wake kumuzunguka, na kuvifunika vilindi vya bahari. |
|
| 31 |
|
| Kwa mvua anawakulisha watu na kuwapatia chakula kwa wingi. |
|
| 32 |
|
| Anaukamata umeme kwa mikono yake, kisha anapiga nao shabaha. |
|
| 33 |
|
| Radi inatangaza kuja kwa Mungu; hata nyama wanajua kwamba anakuja. |
|
|
|
|