|
| 1 |
|
| Halafu Yawe akamujibu Yobu kutoka katika zoruba: |
|
| 2 |
|
| Nani wewe unayevuruga mipango yangu kwa maneno yasiyokuwa na akili? |
|
| 3 |
|
| Ujikaze kama mwanaume, nami nitakuuliza nawe utanijibu. |
|
| 4 |
|
| Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Uniambie, kama una maarifa. |
|
| 5 |
|
| Ni nani aliyeweka vipimo vyake, unajua bila shaka! Au nani aliyenyoosha kamba juu yake kwa kuipima? |
|
| 6 |
|
| Nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la musingi, |
|
| 7 |
|
| nyota za asubui zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapiga vigelegele vya shangwe? |
|
| 8 |
|
| Ni nani aliyefunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka katika vilindi? |
|
| 9 |
|
| Ni nani aliyefunika bahari kwa mawingu na kuiviringishia giza kubwa, |
|
| 10 |
|
| aliyeiwekea bahari mipaka na kuizuia kwa vifungio na milango |
|
| 11 |
|
| na kuiambia: “Mwisho wako ni hapa, si zaidi! Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!” |
|
| 12 |
|
| Yobu, tangu uzaliwe umekwisha kuamuru kupambazuke na kufanya mapambazuko yajue pahali pake, |
|
| 13 |
|
| kusudi yapate kukamata dunia kwa pembe zake na kuwatikisa watenda mabaya? |
|
| 14 |
|
| Dunia inageuka na kupata rangi kama nguo; kama udongo wa mufinyanzi unavyogeuzwa na muhuri. |
|
| 15 |
|
| Lakini waovu watanyimwa mwangaza wao, mukono wanaonyoosha kwa kupiga watu utavunjwa. |
|
| 16 |
|
| Umepata kufika kwenye chemichemi za bahari au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari? |
|
| 17 |
|
| Umekwisha kuonyeshwa milango ya kifo au kuona milango ya makao ya giza kubwa? |
|
| 18 |
|
| Unajua ukubwa wa dunia? Uniambie kama unajua haya yote. |
|
| 19 |
|
| Makao ya mwangaza yako wapi? Kwenye nyumba ya giza ni wapi, |
|
| 20 |
|
| kusudi upate kupeleka kwenye makao yake, na kuifahamu njia ya kwenda kule kwake. |
|
| 21 |
|
| Wewe unapaswa kujua, wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi! |
|
| 22 |
|
| Umekwisha kuingia katika akiba za teluji, au kuona akiba za mvua ya mawe |
|
| 23 |
|
| ambavyo nimeviweka kwa ajili ya wakati wa fujo, kwa ajili ya siku ya mapigano na vita? |
|
| 24 |
|
| Unajua mwangaza unagawanywa kwa njia gani, au namna gani upepo wa mashariki unavyosambazwa katika dunia? |
|
| 25 |
|
| Nani aliyechora katika anga njia kwa ajili ya mvua? Nani aliyeonyesha radi njia yake katika mawingu, |
|
| 26 |
|
| nayo ikasababisha mvua kunyesha katika inchi kusikoishi mutu na katika jangwa ambako hakuna mutu, |
|
| 27 |
|
| kusudi ikunyweshe inchi kavu na yenye kukauka na kuifanya ioteshe majani? |
|
| 28 |
|
| Mvua ina baba? Au nani amezaa matone ya umande? |
|
| 29 |
|
| Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Nani aliyezaa teluji? |
|
| 30 |
|
| Maji yanageuka kuwa magumu kama jiwe, na uso wa bahari unaganda. |
|
| 31 |
|
| Angalia makundi ya nyota: Unaweza kuifunga minyororo Kilimia, au kuviregeza vifungo vya Orioni? |
|
| 32 |
|
| Unaweza kuongoza nyota kwa wakati wake, au kumwongoza Dubu pamoja na vitoto vyake? |
|
| 33 |
|
| Unayajua maagizo ya mbingu? Unaweza kuzipangia utaratibu wao katika dunia? |
|
| 34 |
|
| Unaweza kupiga vigelegele na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mutiririko wa mvua? |
|
| 35 |
|
| Wewe ukiamuru umeme uangaze, utakufikia na kusema: “Nipo hapa”? |
|
| 36 |
|
| Ni nani aliyemujulisha kwarara kujaa kwa muto Nili au aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja? |
|
| 37 |
|
| Nani mwenye akili ya kuweza kuhesabu mawingu au kuinamisha vibuyu vya maji kule katika mbingu |
|
| 38 |
|
| kusudi mavumbi katika dunia yagandamane na udongo ushikamane na kuwa matope? |
|
| 39 |
|
| Unaweza kumwindia simba dike au kuishibisha hamu ya simba wakali |
|
| 40 |
|
| wanapojificha ndani ya matundu yao, au kulala katika maficho wakivizia? |
|
| 41 |
|
| Ni nani anayewapa vibombobombo chakula chao, vitoto vyao vinaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na kule kwa njaa? |
|
|
|
|