|
| 1 |
|
| Unajua mbuzi wa milima anazaa wakati gani, au umekwisha kuona kulungu akizaa? |
|
| 2 |
|
| Unajua anapata mimba kwa muda gani, au siku yenyewe ya kuzaa unaijua? |
|
| 3 |
|
| Wanachutama kwa kuzaa, wanazaa vitoto vyao. |
|
| 4 |
|
| Vitoto vyao vinapata nguvu, vinakomaa kulekule katika pori, kisha vinawaacha wamama zao na kwenda zao. |
|
| 5 |
|
| Nani aliyemwacha huru punda wa pori? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua? |
|
| 6 |
|
| Mimi niliwapa jangwa likuwe nyumba yao, mbuga zenye chumvi kuwa makao yao. |
|
| 7 |
|
| Wanajitenga kabisa na makelele ya miji, hawasikilizi kelele la muchungaji. |
|
| 8 |
|
| Wanatembeatembea katika milima kwa kupata malisho, na kutafuta kitu chochote kinachokuwa kibichi. |
|
| 9 |
|
| Mbogo atakubali kukutumikia? Atakubali kulala katika zizi lako? |
|
| 10 |
|
| Unaweza kumufunga mbogo kamba kwa kulima shamba, au akokote jembe la kulima? |
|
| 11 |
|
| Utamutegemea kwa sababu ana nguvu nyingi na kumwacha akufanyie kazi zako nzito? |
|
| 12 |
|
| Unamutazamia mbogo akuvunie mavuno yako, na kuleta ngano kwenye nafasi ya kupepetea? |
|
| 13 |
|
| Mbuni anapigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hawezi kuruka kama korongo. |
|
| 14 |
|
| Mbuni anayaacha mayai yake juu ya udongo kusudi yapate joto ndani ya muchanga; |
|
| 15 |
|
| lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa, au kuvunjwa na nyama wa pori. |
|
| 16 |
|
| Mbuni anatendea vitoto vyake kwa ukali kama vile si vyake, hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi; |
|
| 17 |
|
| kwa sababu nilimufanya asahau hekima yake, wala sikumupa sehemu yoyote ya akili. |
|
| 18 |
|
| Lakini akianza kukimbia, anamuchekelea hata farasi na mupanda-farasi. |
|
| 19 |
|
| Yobu, ni wewe ndiwe uliyewapa farasi nguvu, ukawavalisha kwenye shingo manyoya marefu? |
|
| 20 |
|
| Ni wewe unayemufanya farasi aruke kama nzige? Mulio wake wa maringo ni wa ajabu! |
|
| 21 |
|
| Anakwaruzakwaruza udongo katika mabonde kwa pupa; anakimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote. |
|
| 22 |
|
| Farasi anaichekelea hofu, na hatishiki; wala upanga hauwezi kumurudisha nyuma. |
|
| 23 |
|
| Silaha wapanda-farasi wanazobeba, zinagongana kwa sauti na kuangaa kwenye jua. |
|
| 24 |
|
| Farasi anasonga mbele, akitetemeka kwa hasira; baragumu inapolia, yeye hasimami. |
|
| 25 |
|
| Kila mara baragumu inapopigwa, yeye anatoa sauti; anasikia harufu ya vita toka mbali, anasikia mushindo wa majemadari wakitoa amri kwa makelele. |
|
| 26 |
|
| Mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka, na kunyoosha mabawa yake kuelekea upande wa kusini? |
|
| 27 |
|
| Tai anapanda juu kwa amri yako, na kuweka chicha yake juu kwenye milima? |
|
| 28 |
|
| Tai anafanya makao yake juu ya mawe marefu, na incha kali za mawe makubwa ndizo maficho yake. |
|
| 29 |
|
| Kutoka kule anavizia nyama, macho yake yanaiona kutoka mbali. |
|
| 30 |
|
| Vitoto vyake vinafyonza damu; pale muzoga unapokuwa ndipo tai anapokuwa. |
|
|
|
|