BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Zaburi ya Daudi. Wimbo wangu unaelekea wema na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Yawe. |
| 2 |
| Nitashikamana na mwenendo mukamilifu. Utakuja kwangu wakati gani? Nitaishi kwa ukamilifu ndani ya nyumba yangu; |
| 3 |
| sitavumilia hata kidogo mambo ya upuuzi. Ninachukia matendo ya watu wapotovu, mimi sitaambatana nayo. |
| 4 |
| Upotovu wowote ukuwe mbali nami; sitahusika kabisa na uovu. |
| 5 |
| Nitateketeza yule anayemuteta mwenzake, sitamuvumilia mwenye majivuno na kiburi. |
| 6 |
| Nitawaangalia waaminifu katika inchi, wapate kuishi pamoja nami. Watu wakamilifu, ndio watakaonitumikia. |
| 7 |
| Mwongo yeyote hatakaa ndani ya nyumba yangu; hakuna musema uongo atakayekaa kwangu. |
| 8 |
| Siku kwa siku nitawaangamiza waovu wote katika inchi; nitawaangamiza wabaya wote katika muji wa Yawe. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/101.mp3
150
101