BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Zaburi ya Daudi: Wimbo. |
| 2 |
| Moyo wangu ni tayari, ee Mungu. Moyo wangu ni tayari. Nitaimba na kukushangilia! Amuka, ee nafsi yangu! |
| 3 |
| Muamuke, enyi kinubi na zeze! Nitaamusha mapambazuko! |
| 4 |
| Ee Yawe, nitakushukuru kati ya mataifa; nitakuimbia sifa kati ya mataifa. |
| 5 |
| Wema wako ni mukubwa kuliko mbingu; uaminifu wako unaenea hata kwenye mawingu. |
| 6 |
| Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu! Utukufu wako uenee katika dunia yote! |
| 7 |
| Ukomboe watu hao unaowapenda; utusaidie kwa mukono wako na kutusikiliza. |
| 8 |
| Mungu amesema toka hekalu lake takatifu: “Sasa nitakwenda kwa shangwe kugawanya Sekemu, bonde la Sukoti nitalipima sehemu sehemu. |
| 9 |
| Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efuraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya kifalme. |
| 10 |
| Moabu ni kama bakuli langu la kunawia; nitatupia kiatu changu katika Edomu kwa kuirizi, nitapiga kelele la ushindi juu ya Wafilistini!” |
| 11 |
| Ni nani atakayenipeleka katika muji unaozungukwa na kuta? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu? |
| 12 |
| Ee Mungu, umetuacha kabisa? Wewe hauendi tena na makundi yetu ya waaskari! |
| 13 |
| Utupatie musaada juu ya waadui zetu, maana musaada wa mwanadamu haufai kitu. |
| 14 |
| Mungu akikuwa upande wetu, tutashinda. Yeye ndiye atakayewaponda waadui zetu. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/108.mp3
150
108