BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Wimbo wa safari za kidini. Katika taabu yangu nilimwita Yawe, naye akanijibu. |
| 2 |
| Uniokoe, ee Yawe, kutoka watu wadanganyifu na waongo. |
| 3 |
| Enyi watu wadanganyifu, mutapewa kitu gani? Mutaazibiwa namna gani? |
| 4 |
| Kwa mishale mikali ya waaskari, kwa makaa ya moto mukali! |
| 5 |
| Ole wangu maana ninaishi kama mugeni huko Meseki; ninaishi kama mugeni katika mahema ya Kedari. |
| 6 |
| Nimeishi muda murefu sana kati ya watu wanaochukia amani! |
| 7 |
| Ninaposema kwamba ninataka amani, wao wanataka tu vita. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/120.mp3
150
120