BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Wimbo wa safari za kidini. Yawe alipoturudisha tena Sayuni, tulikuwa kama watu wanaoota ndoto! |
| 2 |
| Hapo kinywa chetu kilijaa kicheko; tulishangilia kwa furaha. Nao watu wa mataifa mengine walisema: “Yawe amewatendea mambo makubwa!” |
| 3 |
| Kweli Yawe alitutendea maajabu, tulifurahi kweli kweli! |
| 4 |
| Ee Yawe, utengeneze hali yetu, kama vile maji yanavyorudi katika jangwa la Negebu. |
| 5 |
| Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa shangwe. |
| 6 |
| Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia, watarudi kwa furaha wakichukua mavuno. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/126.mp3
150
126