BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kwa mukubwa wa waimbaji: Zaburi ya Daudi. Ninakulilia, ee Yawe, ukuje haraka kunisaidia! Usikilize sauti yangu wakati ninapokuita! |
| 2 |
| Upokee maombi yangu kama ubani; ninapoinua mikono yangu kwako, unikubali kama sadaka ya magaribi. |
| 3 |
| Ee Yawe, ulinde kinywa changu, uweke mulinzi kwenye mulango wa kinywa changu. |
| 4 |
| Unikinge nisielekee kufanya mabaya, nisijishugulishe na matendo maovu, nisijiunge na watu wanaotenda mabaya, wala nisishiriki hata kidogo katika karamu zao. |
| 5 |
| Afazali mutu mwema anipige kwa kunionya; lakini sikubali hata kidogo kusifiwa na wabaya, maana ninaomba siku zote juu ya maovu yao. |
| 6 |
| Wakubwa wao watakapopondwa juu ya mawe, ndipo watatambua kwamba maneno yangu yalikuwa mazuri. |
| 7 |
| Mifupa yao itatawanywa kwenye midomo ya kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! |
| 8 |
| Lakini mimi ninakutegemea, ee Yawe, Mungu wangu; ninakimbilia kwako, usiniache katika hatari. |
| 9 |
| Unikinge na mitego waliyonitegea, uniepushe na wavu wa hao watu waovu. |
| 10 |
| Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe, wakati mimi ninaponyoka. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/141.mp3
150
141