Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako. |
| 2 |
| Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki. |
| 3 |
| Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani. |
| 4 |
| Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. |
| 5 |
| Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. |
| 6 |
| Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. |
| 7 |
| Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni |
| 8 |
| Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu. |
| 9 |
| Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche. |
| 10 |
| Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, |
| 11 |
| Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni; |
| 12 |
| Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/psalms/143.mp3
150
143