Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Ee bwana, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie. |
| 2 |
| Usimhukumu mtumishi wako, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. |
| 3 |
| Adui hunifuatilia, hunipondaponda chini; hunifanya niishi gizani kama wale waliokufa zamani. |
| 4 |
| Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. |
| 5 |
| Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya. |
| 6 |
| Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. |
| 7 |
| Ee bwana, unijibu haraka, roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. |
| 8 |
| Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. Nionyeshe njia nitakayoiendea, kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. |
| 9 |
| Ee bwana, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako. |
| 10 |
| Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare. |
| 11 |
| Ee bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, kwa haki yako nitoe katika taabu. |
| 12 |
| Kwa upendo wako usiokoma, nyamazisha adui zangu; waangamize watesi wangu wote, kwa kuwa mimi ni mtumishi wako. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/psalms/143.mp3
150
143