BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Zaburi ya Daudi. Atukuzwe Yawe, yeye ni: nguvu yangu, yule anayeizoeza mikono yangu kupigana vita na kuvifundisha vidole vyangu kugombana, |
| 2 |
| rafiki yangu wa kweli, kimbilio langu, upango wangu, mukombozi wangu, ngao yangu, yule anayenilinda, yule anayeshinda mataifa na kuyaweka chini yangu. |
| 3 |
| Ee Yawe, mutu ni nini hata umujali? Mwanadamu ni nini hata ufikiri juu yake? |
| 4 |
| Mwanadamu ni kama pumzi tu; siku zake zinapita kama kivuli. |
| 5 |
| Uinamishe mbingu zako, ee Yawe, ushuke chini! Uiguse milima, nayo itoe moshi! |
| 6 |
| Upige umeme, uwasambaze waadui; upige mishale yako, uwakimbize! |
| 7 |
| Unyooshe mukono wako kutoka juu, uniopoe katika maji haya mengi, uniokoe kutoka makucha ya wageni |
| 8 |
| ambao wanasema maneno ya uongo na kunyoosha mukono kwa kushuhudia uongo. |
| 9 |
| Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mupya; nitakupigia kinubi cha nyuzi kumi, |
| 10 |
| wewe unayewapa wafalme ushindi, unayemwokoa mutumishi wako Daudi! |
| 11 |
| Uniokoe kutoka upanga wa waadui wakali, uniokoe kutoka makucha ya wageni, ambao wanasema maneno ya uongo, wanaonyoosha mukono kwa kushuhudia uongo. |
| 12 |
| Katika ujana wao, wana wetu wakuwe kama mimea iliyostawi vizuri; nao wabinti wetu wakuwe wazuri kama nguzo zilizochongwa kwa kupamba nyumba ya kifalme. |
| 13 |
| Gala zetu zijae mavuno ya kila aina. Kondoo wetu katika mbuga wazae maelfu na maelfu. |
| 14 |
| Ngombe wetu wakuwe na afya na nguvu, kusitokwe mimba wala kukosa kuibeba. Kusikuwe tena kilio katika mitaa yetu. |
| 15 |
| Heri taifa ambalo limejaliwa hayo! Heri taifa ambalo Yawe ndiye Mungu wao! |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/144.mp3
150
144