|
| 1 |
|
| Wimbo wa sifa wa Daudi. Nitakutukuza, ee Mungu wangu na mufalme wangu; nitalitukuza jina lako kwa milele na milele. |
|
| 2 |
|
| Nitakutukuza kila siku; nitalisifu jina lako kwa milele na milele. |
|
| 3 |
|
| Yawe ni mukubwa, anastahili sifa nyingi; ukubwa wake hauwezi kuchunguzika. |
|
| 4 |
|
| Sifa za matendo yako zitaelezwa kwa kizazi hata kizazi, watu watatangaza matendo yako makubwa. |
|
| 5 |
|
| Nitasema juu ya utukufu na mamlaka yako, nitafikiri juu ya matendo yako ya ajabu. |
|
| 6 |
|
| Watu watatangaza ukubwa wa matendo yako ya ajabu, nami nitatangaza ukubwa wako. |
|
| 7 |
|
| Watatangaza sifa za uzuri wako mwingi, na kuimba juu ya haki yako. |
|
| 8 |
|
| Yawe ni mwenye huruma na rehema; yeye hakasiriki upesi, amejaa wema. |
|
| 9 |
|
| Yawe ni muzuri kwa wote, ni mwenye huruma kwa viumbe vyake vyote. |
|
| 10 |
|
| Viumbe vyako vyote vitakushukuru, ee Yawe, nao waaminifu wako watakutukuza. |
|
| 11 |
|
| Watasema juu ya utukufu wa ufalme wako, na kutangaza juu ya nguvu yako kubwa, |
|
| 12 |
|
| kusudi kila mutu ajue matendo yako makubwa, na mamlaka ya ufalme wako wenye utukufu. |
|
| 13 |
|
| Ufalme wako ni ufalme wa milele; mamlaka yako yanadumu vizazi vyote. Yawe ni mwaminifu katika ahadi zake zote, ni mwema katika matendo yake yote. |
|
| 14 |
|
| Yawe anawashikilia wote wanaoanguka; anawainua wote waliogandamizwa. |
|
| 15 |
|
| Viumbe vyote vinakutazamia, nawe unavipatia chakula chao kwa wakati wake. |
|
| 16 |
|
| Unafumbua mukono wako kwa moyo safi, unatimiza mahitaji ya kila kiumbe kinachoishi. |
|
| 17 |
|
| Yawe ni mwenye haki katika njia zake zote; ni mwema katika matendo yake yote. |
|
| 18 |
|
| Yawe yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wale wanaomwomba kwa uaminifu. |
|
| 19 |
|
| Anajibia mahitaji yao wote wanaomwabudu; anasikia kilio chao na kuwaokoa. |
|
| 20 |
|
| Yawe anawalinda wote wanaomupenda; lakini anawaangamiza waovu wote. |
|
| 21 |
|
| Nitatangaza sifa za Yawe; viumbe vyote vilisifu jina lake takatifu, kwa milele na milele. |
|
|
|
|