BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Maombi ya Daudi. Ee Yawe, usikie ombi langu la haki, usikilize kilio changu, uyategee sikio maombi yangu yasiyokuwa ya udanganyifu. |
| 2 |
| Haki yangu ikuje kutoka kwako, maana wewe unajua jambo la haki. |
| 3 |
| Wewe unajua kabisa moyo wangu; umenifikia usiku kunichunguza, umenitia katika majaribu; haukuona uovu ndani yangu, sikusema kitu kisichofaa. |
| 4 |
| Juu ya matendo watu wanayotenda, mimi nimetii amri yako, sikushika njia za watesaji wakali. |
| 5 |
| Nimefuata siku zote njia yako; wala sijatereza hata kidogo. |
| 6 |
| Ee Mungu, ninakuita, maana wewe unanijibu; unitegee sikio, uyasikie maneno yangu. |
| 7 |
| Onyesha wema wako wa ajabu; uwaokoe kutoka waadui zao wale wanaokimbilia kwako. |
| 8 |
| Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako, |
| 9 |
| mbali na mashambulio ya waovu, mbali na waadui zangu wa hatari wanaonizunguka. |
| 10 |
| Hao hawana huruma yoyote ndani ya moyo; wamejaa maneno ya kujivuna. |
| 11 |
| Wananifuatilia na kunizunguka; wananivizia waniangushe chini. |
| 12 |
| Wako tayari kunirarua kama simba, kama simba mukali anavyovizia nyama. |
| 13 |
| Ee Yawe, simama sasa uwapiganishe na kuwaporomosha! Kwa upanga wako uokoe nafsi yangu kutoka waovu. |
| 14 |
| Ee Yawe, mukono wako uwafukuze kati ya watu, tukio lao likuwe kutengana na wanaokuwa wazima. Uwashibishe kwa akiba uliyowawekea, watoto wao nao washibe na kuacha sehemu, wawaachie hata na wajukuu wao. |
| 15 |
| Lakini mimi nitauona uso wako, maana mimi ni mutu wa haki; nitakapoamuka nitajaa furaha kwa sababu unanitokea. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/017.mp3
150
17