Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili? |
| 2 |
| Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi |
| 3 |
| Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. |
| 4 |
| Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. |
| 5 |
| Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. |
| 6 |
| Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu. |
| 7 |
| Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. |
| 8 |
| Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. |
| 9 |
| Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi. |
| 10 |
| Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe. |
| 11 |
| Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. |
| 12 |
| Shikeni yaliyo bora |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/psalms/002.mp3
150
2