Bibilia Takatifu 2025
|
| 1 |
| Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na mataifa kula njama bure? |
| 2 |
| Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. |
| 3 |
| Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” |
| 4 |
| Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. |
| 5 |
| Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, |
| 6 |
| “Nimemtawaza mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” |
| 7 |
| Nitatangaza amri ya BWANA: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa. |
| 8 |
| Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako. |
| 9 |
| Utawatawala kwa fimbo ya kifalme ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” |
| 10 |
| Kwa hiyo, ninyi wafalme, iweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. |
| 11 |
| Mtumikieni BWANA kwa hofu na mshangilieni kwa kutetemeka. |
| 12 |
| Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilicontemporary/psalms/002.mp3
150
2