BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Zaburi ya Daudi. Yawe ni muchungaji wangu; sitapungukiwa na kitu. |
| 2 |
| Ananipumzisha kwenye majani mabichi; ananiongoza kando ya maji matulivu, |
| 3 |
| na kuirudishia nafsi yangu nguvu mupya. Ananiongoza katika njia sawa kwa utukufu wa jina lake. |
| 4 |
| Hata nikipita katika bonde la giza kubwa, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe, ee Yawe, ni pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vinanipa moyo. |
| 5 |
| Umenitayarishia karamu mbele ya waadui zangu. Umekipakaa kichwa changu mafuta. Kikombe changu umekijaza tele. |
| 6 |
| Kweli, uzuri na wema wako vitakuwa pamoja nami siku zote za maisha yangu; nami nitakaa katika nyumba ya Yawe milele. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/023.mp3
150
23