|
| 1 |
|
| Zaburi ya Daudi. Ee Yawe, ninakutolea moyo wangu. |
|
| 2 |
|
| Ninakutumainia wewe, ee Mungu wangu, usiniache nifezeheke; waadui zangu wasifurahie kushindwa kwangu. |
|
| 3 |
|
| Usimwache anayekutumainia kupata haya; lakini wafezeheke wote wanaokuasi kwa makusudi. |
|
| 4 |
|
| Unijulishe njia zako, ee Yawe; unifundishe nifuate unayotaka. |
|
| 5 |
|
| Uniongoze katika ukweli wako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu, mwokozi wangu; ninakutegemea wewe kila siku. |
|
| 6 |
|
| Ee Yawe, ukumbuke rehema yako na wema wako ambazo ni za milele. |
|
| 7 |
|
| Usikumbuke zambi na makosa ya ujana wangu; unikumbuke kwa kadiri ya wema wako, kwa ajili ya uzuri wako, ee Yawe. |
|
| 8 |
|
| Yawe ni muzuri na wa usawa, kwa hiyo anawafundisha wakosaji njia. |
|
| 9 |
|
| Anawaongoza wanyenyekevu katika haki; anawafundisha njia yake. |
|
| 10 |
|
| Njia zote za Yawe ni njema na za uaminifu kwa wale wanaoshika agano lake na maagizo yake. |
|
| 11 |
|
| Kwa ajili ya jina lako, ee Yawe, unisamehe kosa langu, kwa maana ni kubwa. |
|
| 12 |
|
| Kila mutu anayemwabudu Yawe, Yawe atamufundisha njia ya kufuata. |
|
| 13 |
|
| Mutu wa namna hiyo atafanikiwa siku zote, na wazao wake watarizi inchi. |
|
| 14 |
|
| Yawe ni rafiki ya wale wanaomwabudu; yeye anawajulisha agano lake. |
|
| 15 |
|
| Ninainua macho kwa Yawe siku zote; yeye ataopoa miguu yangu kutoka mutego. |
|
| 16 |
|
| Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni pekee na zaifu. |
|
| 17 |
|
| Uniondolee mahangaiko ya moyo wangu; uniondoe katika mashaka yangu. |
|
| 18 |
|
| Uangalie mateso yangu na taabu yangu; unisamehe zambi zangu zote. |
|
| 19 |
|
| Angalia jinsi waadui zangu wanavyokuwa wengi; ona jinsi wanavyonichukia vikali. |
|
| 20 |
|
| Uyalinde maisha yangu, uniokoe; ninakukimbilia wewe, usikubali nifezeheke. |
|
| 21 |
|
| Ukamilifu na usawa vinanikinga, maana ninakutumainia wewe. |
|
| 22 |
|
| Ee Mungu, uwaokoe watu wako, Israeli; uwaokoe kutoka taabu zao zote. |
|
|
|
|