Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Ee bwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! |
| 2 |
| Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” |
| 3 |
| Lakini wewe, Ee bwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. |
| 4 |
| Ninamlilia bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. |
| 5 |
| Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana bwana hunitegemeza. |
| 6 |
| Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande. |
| 7 |
| Ee bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu. |
| 8 |
| Kwa maana wokovu watoka kwa bwana. Baraka yako na iwe juu ya watu wako. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/psalms/003.mp3
150
3