×

BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002

Zaburi 30

1
Mashairi yanayoelekea muzinduo wa hekalu. Zaburi ya Daudi.
2
Ninakutukuza, ee Yawe, maana umeniokoa, wala haukuwaacha waadui zangu wanisimange.
3
Ee Yawe, Mungu wangu, nilikulilia, nawe ukaniponyesha.
4
Ee Yawe, umeniokoa kutoka kuzimu; umenipa tena uzima, umenitoa kutoka kati ya wafu.
5
Mumwimbie Yawe sifa, enyi waaminifu wake; mukumbuke utakatifu wake na kumushukuru.
6
Hasira yake inadumu muda kidogo tu, upendo wake unadumu milele. Kilio kinaweza kuwa usiku, lakini muchana kunatokea furaha.
7
Mimi nilipofanikiwa, nilisema: “Sitashindwa hata kidogo!
8
Kwa upendo wako, ee Yawe, umeniimarisha kama mulima mukubwa.” Lakini ukajificha mbali nami, nami nikafazaika.
9
Nilikulilia wewe, ee Yawe; nilikusihi, ee Yawe:
10
“Utapata faida gani nikikufa na kushuka mpaka katika shimo la wafu? Mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu? Yanaweza kusimulia uaminifu wako?
11
Usikie, ee Yawe, unihurumie; ee Yawe, unisaidie!”
12
Wewe umegeuza malalamiko yangu kuwa ngoma ya furaha; umeniondolea huzuni yangu, ukanijaza furaha.
13
Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Yawe, Mungu wangu, nitakushukuru milele.
Swahili Bible 2002
Bible in Swahili Congo Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002
:
Hifadhi Vidokezo