BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi, mutumishi wa Yawe. |
| 2 |
| Zambi inaongea na mutu mwovu, ndani kabisa ya moyo wake; kuogopa Mungu si kitu kwake. |
| 3 |
| Mwovu anajipendelea mwenyewe, anafikiri uovu wake hautagunduliwa na kulaaniwa. |
| 4 |
| Kila anachosema ni uovu na uongo; ameacha kutumia hekima na kutenda mema. |
| 5 |
| Anapolala anawaza kutenda maovu, anajiweka katika njia isiyokuwa nzuri, wala hachukii uovu. |
| 6 |
| Wema wako, ee Yawe, unaenea hata mbinguni; uaminifu wako unafika hata kwenye mawingu. |
| 7 |
| Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Yawe, unawalinda wanadamu na nyama. |
| 8 |
| Kweli wema wako ni bora! Wanadamu wanakimbilia kwenye kivuli cha mabawa yako. |
| 9 |
| Unawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako; unawakunywesha katika muto wa wema wako. |
| 10 |
| Wewe ndiwe asili ya uzima; kwa mwangaza wako tunaona mwangaza. |
| 11 |
| Uendelee kuwatendea mema wale wanaokutambua; uzidi kuokoa wenye moyo wenye kunyooka. |
| 12 |
| Usikubali wenye majivuno wanishambulie, wala watu waovu wanikimbize. |
| 13 |
| Kumbe watenda maovu wameanguka; wameangushwa chini, hawawezi kuinuka. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/036.mp3
150
36