Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu. |
| 2 |
| Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini? |
| 3 |
| Fahamuni hakika kwamba bwana amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; bwana atanisikia nimwitapo. |
| 4 |
| Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu. |
| 5 |
| Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni bwana. |
| 6 |
| Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee bwana, tuangazie nuru ya uso wako. |
| 7 |
| Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. |
| 8 |
| Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee bwana, waniwezesha kukaa kwa salama. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/psalms/004.mp3
150
4