BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Usiharibu.” Mashairi ya Daudi alipomuponyoka Saulo na kujificha katika pango. |
| 2 |
| Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana ninakukimbilia wewe. Ninakimbilia kwenye kivuli cha mabawa yako, mpaka zoruba ya maangamizi ipite. |
| 3 |
| Ninamulilia Mungu Mukubwa, Mungu anayenikamilishia nia yake. |
| 4 |
| Atanipelekea musaada toka mbinguni na kuniokoa, atawafezehesha hao wanaonishambulia. Mungu atanionyesha wema na uaminifu wake! |
| 5 |
| Mimi nimezungukwa na waadui, wenye uchu wa damu kama simba; meno yao ni kama mikuki na mishale, ndimi zao ni kama panga kali. |
| 6 |
| Utukuzwe, ee Mungu, juu katika mbingu! Utukufu wako uenee katika dunia yote! |
| 7 |
| Waadui wamenitegea wavu waninase, nami ninaugua kwa huzuni. Wamenichimbia shimo katika njia yangu, lakini wao wenyewe wametumbukia humo. |
| 8 |
| Moyo wangu ni tayari, ee Mungu, moyo wangu ni tayari; nitaimba na kukushangilia! |
| 9 |
| Amuka, ee nafsi yangu! Muamuke, enyi kinubi na zeze! Nitayaamusha mapambazuko! |
| 10 |
| Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu; nitakuimbia sifa kati ya mataifa. |
| 11 |
| Wema wako unaenea hata juu katika mbingu, uaminifu wako unafika hata katika mawingu. |
| 12 |
| Utukuzwe, ee Mungu, juu katika mbingu! Utukufu wako uenee katika dunia yote! |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/057.mp3
150
57