BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi inayoelekea sadaka yake ya ukumbusho. |
| 2 |
| Ee Mungu, uniokoe! Ee Yawe, ukuje haraka unisaidie. |
| 3 |
| Wapate haya na kufezeheka wanaotaka kuniua! Warudi nyuma na kufezeheka wanaonitakia hasara! |
| 4 |
| Wapumbazike kwa haya, hao wanaofurahia kunizomea! |
| 5 |
| Lakini wote wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wote wanaopenda wokovu wako, waseme siku zote: “Mungu ni mukubwa!” |
| 6 |
| Nami ninayekuwa masikini na mukosefu, unifikie haraka, ee Mungu! Wewe ndiwe musaada wangu na mukombozi wangu. Ee Yawe, usikawie! |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/070.mp3
150
70