BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Maombi ya Musa, mutu wa Mungu. Ee Bwana, tangia vizazi vyote, wewe umekuwa usalama wetu. |
| 2 |
| Mbele milima haijakuwa, mbele haujauumba ulimwengu, wewe ndiwe Mungu, milele na milele. |
| 3 |
| Unawarudisha watu katika mavumbi walimotoka, ukisema: “Wanadamu, murudi!” |
| 4 |
| Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha pita, ni kama makesha ya usiku mumoja. |
| 5 |
| Unatowesha mbali watu kama ndoto! Wanadamu ni kama majani yanayochipuka asubui: |
| 6 |
| asubui yanachipuka na kuchanua, magaribi yamekwisha nyauka na kukauka. |
| 7 |
| Hasira yako inatuangamiza; tunatishwa na kasirani yako. |
| 8 |
| Maovu yetu umeyaweka mbele yako; zambi zetu za siri ziko wazi mbele yako. |
| 9 |
| Kwa hasira yako maisha yetu yanatoweka, yanaisha kama pumzi. |
| 10 |
| Muda wa maisha yetu ni miaka makumi saba, au tukikuwa wenye afya, miaka makumi nane; lakini yote ni shida na taabu! Siku zinapita mbio, nasi tunatoweka! |
| 11 |
| Nani anayetambua uzito wa hasira yako? Nani anayeona matokeo ya kasirani yako? |
| 12 |
| Utufundishe ufupi wa maisha yetu kusudi tuweze kuwa na hekima. |
| 13 |
| Ee Yawe, urudie! Utakasirika mpaka wakati gani? Utuonee huruma sisi watumishi wako. |
| 14 |
| Utushibishe wema wako kila asubui, tupate kushangilia na kufurahi maisha yetu yote. |
| 15 |
| Utujalie sasa miaka mingi ya furaha, kama ulivyotupa miaka mingi ya shida na taabu. |
| 16 |
| Utuonyeshe matendo yako sisi watumishi wako; uwaonyeshe wazao wetu utukufu wako. |
| 17 |
| Utuonyeshe uzuri wako, ee Bwana, Mungu wetu; uimarishe kazi zetu, uziimarishe. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/psalms/090.mp3
150
90