|
| 1 |
|
| Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, |
|
| 2 |
|
| kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, |
|
| 3 |
|
| na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu, |
|
| 4 |
|
| na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, |
|
| 5 |
|
| ndipo utakapoelewa kumcha bwana na kupata maarifa ya Mungu. |
|
| 6 |
|
| Kwa maana bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. |
|
| 7 |
|
| Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, |
|
| 8 |
|
| kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. |
|
| 9 |
|
| Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki na sawa: yaani kila njia nzuri. |
|
| 10 |
|
| Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako. |
|
| 11 |
|
| Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda. |
|
| 12 |
|
| Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, |
|
| 13 |
|
| wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza, |
|
| 14 |
|
| wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya, |
|
| 15 |
|
| ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao. |
|
| 16 |
|
| Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya, |
|
| 17 |
|
| aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu. |
|
| 18 |
|
| Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa. |
|
| 19 |
|
| Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima. |
|
| 20 |
|
| Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki. |
|
| 21 |
|
| Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. |
|
| 22 |
|
| Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watang’olewa kutoka humo. |
|
|
: |
| 1 | | 2 | | 3 | | 4 | | 5 | | 6 | | 7 | | 8 | | 9 | | 10 | | 11 | | 12 | | 13 | | 14 | | 15 | | 16 | | 17 | | 18 | | 19 | | 20 | | 21 | | 22 | 1
1
1 |
|
|---|
|
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/proverbs/002.mp3
31
2