Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Mpenzi wako amekwenda wapi, ewe mzuri kupita wanawake wote? Mpenzi wako amegeukia njia ipi, tupate kumtafuta pamoja nawe? |
| 2 |
| Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake, kwenye vitalu vya vikolezo, kujilisha bustanini na kukusanya yungiyungi. |
| 3 |
| Mimi ni wake mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; yeye hujilisha katikati ya yungiyungi. |
| 4 |
| Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa, upendezaye kama Yerusalemu, umetukuka kama jeshi lenye bendera. |
| 5 |
| Uyageuze macho yako mbali nami, yananigharikisha. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi wanaoteremka kutoka Gileadi. |
| 6 |
| Meno yako ni kama kundi la kondoo watokao kuogeshwa. Kila mmoja ana pacha lake, hakuna hata mmoja aliye peke yake. |
| 7 |
| Mashavu yako nyuma ya shela yako ni kama vipande viwili vya komamanga. |
| 8 |
| Panaweza kuwepo malkia sitini, masuria themanini na mabikira wasiohesabika; |
| 9 |
| lakini hua wangu, mkamilifu wangu, ni wa namna ya pekee, binti pekee kwa mama yake, kipenzi cha yeye aliyemzaa. Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa; malkia na masuria walimsifu. |
| 10 |
| Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko, mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, ametukuka kama nyota zifuatanazo? |
| 11 |
| Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi ili kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechipua au kama mikomamanga imechanua maua. |
| 12 |
| Kabla sijang’amua, shauku yangu iliniweka katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu. |
| 13 |
| Rudi, rudi, ee Mshulami; rudi, rudi ili tupate kukutazama! Kwa nini kumtazama Mshulami, kama kutazama ngoma ya Mahanaimu? |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/songofsolomon/006.mp3
8
6