Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika mitalawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi; |
| 2 |
| Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro; |
| 3 |
| Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Ambao ni mapacha ya paa; |
| 4 |
| Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski; |
| 5 |
| Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungu yake. |
| 6 |
| Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa! |
| 7 |
| Kimo chako kimefanana na mtende, Na maziwa yako na vichala. |
| 8 |
| Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera; |
| 9 |
| Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao. |
| 10 |
| Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu. |
| 11 |
| Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. |
| 12 |
| Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu. |
| 13 |
| Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/songofsolomon/007.mp3
8
7