Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” |
| 2 |
| Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami. |
| 3 |
| Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. |
| 4 |
| Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema bwana Mwenyezi.’ |
| 5 |
| Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. |
| 6 |
| Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi. |
| 7 |
| Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi. |
| 8 |
| Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiwe mwenye kuasi kama hiyo nyumba ya kuasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.” |
| 9 |
| Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na ukurasa wa kitabu, |
| 10 |
| ambao aliukunjua mbele yangu. Pande zote mbili ulikuwa umeandikwa maneno ya maombolezo, vilio na ole. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/ezekiel/002.mp3
48
2