BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Israeli alipokuwa mutoto, nilimupenda. Kutoka Misri nilimwita mwana wangu. |
| 2 |
| Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita, ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami; waliendelea kuyatambikia Mabali, na kuvifukizia ubani sanamu za miungu. |
| 3 |
| Mimi ndiye niliyemufundisha watu wa Efuraimu kutembea! Mimi mwenyewe niliwatwaa katika mikono yangu; lakini hawakutambua kwamba mimi ndiye niliyewatunza. |
| 4 |
| Niliwaongoza kwa huruma, nilishikamana nao kwa upendo; kama baba anavyomunyanyua mutoto mpaka kwenye shavu lake, ndivyo nami nilivyokuwa kwao. Mimi niliinama chini na kuwakulisha. |
| 5 |
| Basi, watarudi katika inchi ya Misri; watatawaliwa na mufalme wa Asuria, kwa sababu wamekataa kunirudilia. |
| 6 |
| Upanga utavuma katika miji yao, utavunjavunja miimo ya milango yake na kuwaangamiza katika kuta zao. |
| 7 |
| Watu wangu wamekusudia kuniacha mimi, wakiitwa kusimama wapande juu, hakuna hata mumoja anayeweza. |
| 8 |
| Ewe Efuraimu, ninaweza kukuacha namna gani? Ninaweza kukutupilia, ewe Israeli namna gani? Nitaweza namna gani kukufanya kama muji wa Adama? Nitaweza namna gani kukutendea kama Zeboimu! Ninazuizwa na moyo wangu; huruma yangu imezidi kuwa motomoto. |
| 9 |
| Nitaizuia hasira yangu kali; sitamwangamiza tena Efuraimu, maana mimi ni Mungu, wala si mwanadamu. Mimi ndimi Mutakatifu kati yenu, nami sitakuja kuwaangamiza. |
| 10 |
| Watanifuata mimi Yawe ninayenguruma kama simba; nitakaponguruma watanifikia toka magaribi wakitetemeka. |
| 11 |
| Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege, wataruka kutoka Asuria kama njiwa nami nitawarudisha kwao. –Ni ujumbe wa Yawe. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/hosea/011.mp3
14
11