Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. |
| 2 |
| Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. |
| 3 |
| Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi. |
| 4 |
| Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. |
| 5 |
| Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga. |
| 6 |
| Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa. |
| 7 |
| Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana. |
| 8 |
| Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu. |
| 9 |
| Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana. |
| 10 |
| Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi. |
| 11 |
| Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/hosea/006.mp3
14
6