“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng'ombe kutoka katika kundi, akiwa dume au jike, atamleta huyo mbele za BWANA mnyama asiye na dosari.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa BWANA kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.