Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Sikia neno hili, ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi: |
| 2 |
| “Bikira Israeli ameanguka, kamwe hatainuka tena, ameachwa pweke katika nchi yake, hakuna yeyote wa kumwinua.” |
| 3 |
| Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.” |
| 4 |
| Hili ndilo bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi; |
| 5 |
| msitafute Betheli, msiende Gilgali, msisafiri kwenda Beer-Sheba. Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni, na Betheli itafanywa kuwa si kitu.” |
| 6 |
| Mtafuteni bwana mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yusufu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima. |
| 7 |
| Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu na kuiangusha haki chini |
| 8 |
| (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: bwana ndilo jina lake; |
| 9 |
| yeye hufanya maangamizo kwenye ngome na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa), |
| 10 |
| mnamchukia yule akemeaye mahakamani, na kumdharau yule ambaye husema kweli. |
| 11 |
| Mnamgandamiza maskini na kumlazimisha awape nafaka. Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari, hamtaishi ndani yake; ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, hamtakunywa divai yake. |
| 12 |
| Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu. Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa na kuzuia haki ya maskini mahakamani. |
| 13 |
| Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo, kwa kuwa nyakati ni mbaya. |
| 14 |
| Tafuteni mema, wala si mabaya, ili mpate kuishi. Ndipo bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo yupo nanyi. |
| 15 |
| Yachukieni maovu, yapendeni mema; dumisheni haki mahakamani. Yamkini bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atawahurumia mabaki ya Yusufu. |
| 16 |
| Kwa hiyo hili ndilo Bwana, bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza. |
| 17 |
| Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, kwa kuwa nitapita katikati yenu,” asema bwana. |
| 18 |
| Ole wenu ninyi mnaoitamani siku ya bwana! Kwa nini mnaitamani siku ya bwana? Siku hiyo itakuwa giza, si nuru. |
| 19 |
| Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba kumbe akakutana na dubu, kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, kumbe akaumwa na nyoka. |
| 20 |
| Je, siku ya bwana haitakuwa giza, na si nuru: giza nene, bila mwonzi wa mwanga? |
| 21 |
| “Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; siwezi kuvumilia makusanyiko yenu. |
| 22 |
| Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, sitazikubali. Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, sitazitambua. |
| 23 |
| Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu. |
| 24 |
| Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! |
| 25 |
| “Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli? |
| 26 |
| Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu, Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe. |
| 27 |
| Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,” asema bwana, ambaye jina lake ni Mungu Mwenye Nguvu Zote. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/amos/005.mp3
9
5