Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, |
| 2 |
| Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu. |
| 3 |
| Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. |
| 4 |
| Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. |
| 5 |
| Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; |
| 6 |
| Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, |
| 7 |
| Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu. |
| 8 |
| Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; |
| 9 |
| Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana. |
| 10 |
| Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/jonah/002.mp3
4
2