Bibilia Takatifu 2025
|
| 1 |
| Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba BWANA Mungu wake. |
| 2 |
| Akasema: “Katika shida yangu nalimwita BWANA, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu. |
| 3 |
| Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka, mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu. |
| 4 |
| Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako, hata hivyo nitatazama tena kuelekea Hekalu lako takatifu.’ |
| 5 |
| Maji yaliyonimeza yalinitisha, kilindi kilinizunguka; mwani ulijisokota kichwani pangu. |
| 6 |
| Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee BWANA Mungu wangu. |
| 7 |
| “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, BWANA, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. |
| 8 |
| “Wale watu wanaong'ang'ana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao. |
| 9 |
| Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea dhabihu. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa BWANA.” |
| 10 |
| Basi BWANA akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilicontemporary/jonah/002.mp3
4
2