BIBLIA Maandiko Matakatifu 2002
|
| 1 |
| Kisha, Yawe akaamuru samaki mukubwa amumeze Yona, naye akabaki ndani ya tumbo la samaki huyo kwa muda wa siku tatu, usiku na muchana. |
| 2 |
| Basi, Yona akiwa ndani ya tumbo la samaki yule, akamwomba Yawe Mungu wake, |
| 3 |
| akisema: Kwa sababu ya taabu yangu, nilikuomba, ee Yawe, nawe ukanisikiliza; toka chini kuzimu, nilikulilia, nawe ukasikiliza kilio changu. |
| 4 |
| Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari, maji mengi yakanizunguka, mawimbi na maji mengi vikapita juu yangu. |
| 5 |
| Nilizani kwamba nimetupwa mbali nawe; nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu. |
| 6 |
| Maji yalinizunguka na kunisonga; kilindi kilinifikia kila upande, majani ya bahari yakanifunika kichwa. |
| 7 |
| Niliteremuka mpaka kwenye misingi ya milima, katika inchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Yawe, Mungu wangu, umenipandisha nikiwa muzima kutoka mule ndani ya shimo. |
| 8 |
| Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Yawe, maombi yangu yakakufikia katika hekalu lako takatifu. |
| 9 |
| Watu wanaoabudu sanamu za miungu ya bure, wanautupilia mbali uaminifu wao kwako. |
| 10 |
| Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea sadaka, na kutimiza viapo vyangu. Yawe, ndiye anayeokoa. |
| 11 |
| Basi, Yawe akamwamuru yule samaki, naye akamutapika Yona kwenye inchi kavu. |
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahiliswc02/jonah/002.mp3
4
2