Mnajilisha kwa nyama ya watu wangu mnawachuna ngozi yao, mnaivunjavunja mifupa yao, na kuwakatakata kama nyama ya kupika, kama nyama ya kutia ndani ya chungu.
Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu:
Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao.
Sikieni jambo hili enyi viongozi wa wazawa wa Yakobo, sikilizeni, enyi watawala wa Waisraeli: Nyinyi mnachukia mambo ya haki na kupotosha mambo ya adili.
Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!”