Mwenyezi-Mungu anamrudishia Yakobo fahari yake, naam, anawapa tena Waisraeli fahari yao, ingawa wavamizi hawakuwaachia kitu, hata matawi yao ya mizabibu waliyakata.
Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, askari wake wamevaa mavazi mekundu sana. Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto, yamepangwa tayari kushambulia; farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.
Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?
Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akawakamatia simba majike mawindo yao; ameyajaza mapango yake mawindo, na makao yake mapande ya nyama.
Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.