Habari Njema 2001
|
| 1 |
| Kauli ya Mungu aliyoiona nabii Habakuki. |
| 2 |
| “Ee Mwenyezi-Mungu, nitakulilia mpaka lini, nawe usinisikilize na kunisaidia? Kwa nini nalia: ‘Dhuluma’ nawe hutuokoi? |
| 3 |
| Kwa nini wanifanya nishuhudie mabaya na taabu? Uharibifu na ukatili vinanizunguka, ugomvi na mashindano yanazuka. |
| 4 |
| Hivyo sheria haina nguvu, wala haki haitekelezwi. Waovu wanawazunguka waadilifu, hivyo hukumu hutolewa ikiwa imepotoshwa.” |
| 5 |
| Mungu akasema: “Yaangalie mataifa, uone! Utastaajabu na kushangaa. Maana ninatenda kitu ukiwa bado unaishi, kitu ambacho ungeambiwa hungesadiki. |
| 6 |
| Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine. |
| 7 |
| Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha; wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama. |
| 8 |
| “Farasi wao ni wepesi kuliko chui; wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa. Wapandafarasi wao wanatoka mbali, wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo. |
| 9 |
| “Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga. |
| 10 |
| Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka. |
| 11 |
| Kisha wanasonga mbele kama upepo, wafanya makosa na kuwa na hatia, maana, nguvu zao ndizo mungu wao!” |
| 12 |
| “Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu! |
| 13 |
| Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao? |
| 14 |
| “Umewafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe vitambaavyo visivyo na kiongozi! |
| 15 |
| Wakaldayo huwavua watu kwa ndoana, huwavutia nje kwa wavu wao, huwakusanya wote katika jarife lao, kisha hufurahi na kushangilia. |
| 16 |
| Kwa hiyo, wanazitambikia nyavu zao, na kuzifukizia ubani; maana kwa hizo huweza kuishi kwa anasa, na kula chakula cha fahari. |
| 17 |
| “Je, hawataacha kamwe kuvuta upinde wao? Je, wataendelea tu kuwanasa watu, na kuyaangamiza mataifa bila huruma? |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili2001/habakkuk/001.mp3
3
1