Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako, juu ya matendo yako, nami naogopa. Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu; uyafanye yajulikane wakati huu wetu. Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako!
Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.
Nasikia hayo nami ninashtuka mwilini, midomo yangu inatetemeka kwa hofu; mifupa yangu inateguka, miguu yangu inatetemeka. Ninangojea kwa utulivu siku ile ya maafa, ambayo inawajia wale wanaotushambulia.
Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini,