Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| bwana akamwambia Musa, |
| 2 |
| “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.” |
| 3 |
| Hivyo kwa agizo la bwana Musa akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. |
| 4 |
| Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri; |
| 5 |
| kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; |
| 6 |
| kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune; |
| 7 |
| kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu; |
| 8 |
| kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni; |
| 9 |
| kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu; |
| 10 |
| kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi, |
| 11 |
| kutoka kabila la Manase (kabila la Yusufu), Gadi mwana wa Susi; |
| 12 |
| kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali; |
| 13 |
| kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli; |
| 14 |
| kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi; |
| 15 |
| kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. |
| 16 |
| Haya ndiyo majina ya watu ambao Musa aliwatuma kuipeleleza nchi. (Musa akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.) |
| 17 |
| Musa alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. |
| 18 |
| Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi. |
| 19 |
| Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? |
| 20 |
| Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.) |
| 21 |
| Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi. |
| 22 |
| Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.) |
| 23 |
| Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini. |
| 24 |
| Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko. |
| 25 |
| Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. |
| 26 |
| Wakarudi kwa Musa, Haruni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi. |
| 27 |
| Wakampa Musa taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. |
| 28 |
| Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki. |
| 29 |
| Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.” |
| 30 |
| Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Musa na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.” |
| 31 |
| Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.” |
| 32 |
| Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. |
| 33 |
| Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.” |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/numbers/013.mp3
36
13