Habari Njema 2001
|
| 1 |
| Baada ya yale maradhi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, |
| 2 |
| “Hesabuni jumuiya yote ya Waisraeli, kila mtu kufuatana na jamaa yake. Wahesabuni watu wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi wanaofaa kwenda jeshini.” |
| 3 |
| Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, |
| 4 |
| “Hesabuni watu kuanzia na wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.” Idadi ya Waisraeli waliotoka Misri ni hii: |
| 5 |
| Kwanza ni kabila la Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Henoki, Palu, |
| 6 |
| Hesroni na Karmi. |
| 7 |
| Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730. |
| 8 |
| Wazawa wa Palu walikuwa Eliabu, |
| 9 |
| na wanawe Nemueli, Dathani na Abiramu. (Hawa wawili: Dathani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa miongoni mwa jumuiya, lakini wakampinga Mose na Aroni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Mwenyezi-Mungu. |
| 10 |
| Wakati huo ardhi ilifunguka ikawameza, wakafa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu 250; wakawa onyo kwa watu. |
| 11 |
| Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.) |
| 12 |
| Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini, |
| 13 |
| Zera na Shauli. |
| 14 |
| Hizo ndizo koo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume 22,000. |
| 15 |
| Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Shuni, |
| 16 |
| Ozni, Eri, |
| 17 |
| Arodi na Areli. |
| 18 |
| Hizo ndizo koo za kabila la Gadi, jumla wanaume 40,500. |
| 19 |
| Kabila la Yuda lilikuwa na wanawe wa Yuda Eri na Onani. Hawa walifia nchini Kanaani. |
| 20 |
| Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Shela, Peresi, na Zera. |
| 21 |
| Kutoka kwa Peresi, familia ya Hesroni na Hamuli. |
| 22 |
| Hizo ndizo koo za Yuda, jumla wanaume 76,500. |
| 23 |
| Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva, |
| 24 |
| Yashubu na wa Shimroni. |
| 25 |
| Hizo ndizo koo za Isakari, jumla wanaume 64,300. |
| 26 |
| Kabila la Zebuluni lilikuwa na jamaa za Seredi, wa Eloni na wa Yaleeli. |
| 27 |
| Hizo ndizo koo za Zebuluni, jumla wanaume 60,500. |
| 28 |
| Kabila la Yosefu baba yao Manase na Efraimu. |
| 29 |
| Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. |
| 30 |
| Yezeri, Heleki, |
| 31 |
| Asrieli, Shekemu, |
| 32 |
| Shemida na Heferi. |
| 33 |
| Selofehadi, mwana wa Heferi hakupata watoto wa kiume bali wa kike tu, nao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza. |
| 34 |
| Hizo ndizo koo za Manase, jumla wanaume 52,700. |
| 35 |
| Kabila la Efraimu lilikuwa na jamaa za Shuthela, Bekeri na Tahani. |
| 36 |
| Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Shuthela. |
| 37 |
| Hizo ndizo koo za Efraimu, jumla wanaume 32,500. Zote hizo zilitokana na Yosefu. |
| 38 |
| Kabila la Benyamini lilikuwa na jamaa za Bela, Ashbeli, Ahiramu, |
| 39 |
| Shufamu na Hufamu. |
| 40 |
| Koo za Ardi na Naamani, zilitokana na Bela. |
| 41 |
| Hizo ndizo koo za Benyamini, jumla wanaume 45,600. |
| 42 |
| Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; |
| 43 |
| ukoo ulikuwa na wanaume 64,400. |
| 44 |
| Kabila la Asheri lilikuwa na jamaa za Imna, Ishvi na Beria. |
| 45 |
| Koo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria. |
| 46 |
| Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera. |
| 47 |
| Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400. |
| 48 |
| Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni, |
| 49 |
| Yeseri na Shilemu. |
| 50 |
| Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400. |
| 51 |
| Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730. |
| 52 |
| Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, |
| 53 |
| “Makabila haya yatagawiwa nchi iwe urithi wao, kulingana na idadi ya majina yao. |
| 54 |
| Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake. |
| 55 |
| Hata hivyo ugawaji wa nchi utafanywa kwa kura. Kila kabila litarithi kulingana na majina ya ukoo wao. |
| 56 |
| Urithi wa kila kabila utagawanywa kwa kura, kila kabila litapata kulingana na ukubwa au udogo wake.” |
| 57 |
| Hizi ndizo koo za Walawi zilizoorodheshwa na jamaa zao: Gershoni, Kohathi na Merari, |
| 58 |
| Pamoja na jamaa za Libni, Hebroni, Mahli, Mushi na Kora. Kohathi alikuwa baba yake Amramu. |
| 59 |
| Mkewe Amramu aliitwa Yokebedi binti yake Lawi, aliyezaliwa Misri. Huyu alimzalia Amramu watoto wawili wa kiume, Aroni na Mose, na binti mmoja, Miriamu. |
| 60 |
| Aroni alikuwa na watoto wa kiume wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. |
| 61 |
| Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya moto usiofaa. |
| 62 |
| Idadi ya Walawi wanaume wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ilikuwa 23,000. Hawa hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu wao hawakupewa urithi wowote miongoni mwao. |
| 63 |
| Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko. |
| 64 |
| Miongoni mwao hakuwamo hata mtu mmoja aliyesalia kati ya wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni ambao walifanya sensa ya kwanza jangwani Sinai. |
| 65 |
| Mwenyezi-Mungu alikuwa amesema kwamba wote watafia jangwani, na kweli hakuna hata mmoja wao aliyebaki hai, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili2001/numbers/026.mp3
36
26