Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema, |
| 2 |
| Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. |
| 3 |
| Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. |
| 4 |
| Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. |
| 5 |
| Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; |
| 6 |
| nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. |
| 7 |
| Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. |
| 8 |
| Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. |
| 9 |
| Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. |
| 10 |
| Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni. |
| 11 |
| Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. |
| 12 |
| Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. |
| 13 |
| Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. |
| 14 |
| Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache. |
| 15 |
| Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. |
| 16 |
| Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. |
| 17 |
| Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo? |
| 18 |
| Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? |
| 19 |
| Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. |
| 20 |
| Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii? |
| 21 |
| Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. |
| 22 |
| Waliposikia, walistaajabu, wakamwacha, wakaenda zao. |
| 23 |
| Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, |
| 24 |
| wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. |
| 25 |
| Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. |
| 26 |
| Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. |
| 27 |
| Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. |
| 28 |
| Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye. |
| 29 |
| Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. |
| 30 |
| Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. |
| 31 |
| Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, |
| 32 |
| Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. |
| 33 |
| Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake. |
| 34 |
| Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. |
| 35 |
| Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; |
| 36 |
| Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? |
| 37 |
| Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. |
| 38 |
| Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. |
| 39 |
| Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. |
| 40 |
| Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. |
| 41 |
| Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? |
| 42 |
| Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. |
| 43 |
| Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, |
| 44 |
| Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? |
| 45 |
| Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? |
| 46 |
| Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/matthew/022.mp3
28
22